TIMU YA ETO'O YAMTAKA VIDIC

NEMANJA VIDIC amejikuta katika mshituko, baada ya matajiri wa timu ya Anzhi Makhachkala, kudai watatoa kiasi cha pauni milioni 25 kwa ajili ya kumtwaa. Warusi hao wanataka kufanya kweli kama walivyofanya kwa Samuel Eto’o ambaye walimtwaa kwa pauni milioni 20 kutoka Inter na iwapo watafanikiwa hilo watamfanya Vidic ni beki ghali zaidi duniani.
Beki huyo Vidic, 29, ndiye chaguo namba moja la la Warusi hao ambao wamedai wanataka kuhakikisha kila kitu kinakamilika kabla ya dirisha la usajili halijafungwa leo usiku.
Inadaiwa Alex Ferguson amechanganyikiwa na ofa hiyo na kwa sasa anatarajiwa kutoa maamuzi ya mwisho kabla ya dirisha kufungwa la kukubali kumuuza au la.
Anzhi kwa sasa inaongozwa na bilionea wa Kirusi, Suleyman Kerimou, ambaye ameamua kuwekeza zaidi katika timu hiyo. Hivi karibuni alishitua dunia pale aliposema tamlipa Eto’opauni 300,000 kwa wiki.

Comments