TIMBE ARUDI KWAO KUSAKA UBANI, KIIZA,NIYONZIMA NAO WATIMKA

BAADA ya kuanza vibaya kwenye ligi kuu bara kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo Sam Timbe amekwenda kwao nchini Uganda kwa mapumziko mafupi ba atarejea wiki ijayo.

Kwa kipindi ambacho kocha huiyo hatokuwepo nafasi yake itashikwa na kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro .
Aidha nyota wa kimataifa wa timu hiyo Haruna Niyonzima wa Rwanda na Hamis Kiiza wa Uganda kwa ajili ya kujiunga na timu zao za Taifa.
Wakati Kiiza akiondoka  kwa ajili ya kuitumikia timu ya vijana chini ya miaka 23 itakayoshiriki mashindano ya All Africa Games yanayotarajia kuanza Septemba 3-18 jijini Maputo Msumbiji , Niyonzima ameitwa na kwenye timu ya Taifa ya Rwanda.

Comments