TFF WAJISAFISHA KUKOSA FIFA DAY


KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amevunja ukimya na kudai TFF isibebeshwe lawama kwa sababu Taifa Stars imeshindwa kwenda Sudan kwa kuwa Shirikisho la Soka la Sudan (SFA) ndiyo lililoshindwa kuwatumia TFF fedha za tiketi.

Osiah aliyasema hayo jana ikiwa ni siku moja baada ya TFF kutangaza kuifuta ratiba ya mchezo huo uliokuwa ufanyike Agosti 10 mjini Khartoum kwa mujibu wa kalenda ya Fifa baada ya kukosekana tiketi za ndege za kuipeleka timu hiyo nchini Sudan.



Comments