TASWA YALAANI WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO KUBUGHUDHIWA UWANJANI

TASWA inalaani vitendo vya baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu ambao si wastaarabu kuwabughudhi waandishi wa habari za michezo kwa namna mbalimbali wakati wakitekeleza majukumu yao viwanjani na kuwasababishia kwa kiasi fulani washindwe kuyatekeleza kwa ufasaha majukumu hayo.


Matatizo makubwa yameibuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kamati inaona yanasababishwa na kutokuwepo eneo maalum la kukaa waandishi uwanjani, hivyo kujichanganya na mashabiki jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Kutokana na msingi huo kikao kiliiagiza Sekretarieti ya TASWA ifanye mazungumzo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusiana na eneo ambalo lilioneshwa miaka ya nyuma kabla uwanja haujaanza kutumika kwamba ni maalum kwa ajili ya kukaa waandishi wa habari za michezo, ili isaidie kupunguza matatizo hayo.

Comments