TAJIRI ETO'O AANZA NA MOTO URUSI


Anzhi's star rookie Samuel Eto'o (C) scores against Rostov (Image from fc-anji.ru)
Mshambuliaji mpya wa Anzhi, Samuel Eto'o (katikati) akifunga bao lake la kwanza Urusi.

Mchezaji ghali duniani, Samuel Eto’o amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Urusi usiku huu na kuinusuru klabu yake mpya,  Anzhi kufungwa kwa kuipa sare ya 1-1 na Rostov.
­Timu hizo zilikuwa hazijafungana hadi kocha wa Anzhi, Gadzhi Gadzhiev alipomuingiza Eto’o uwanjani dakika ya58.
Ilionekana kana kwamba mwanasoka huyo wa 'bei chafu' dunia nzima angeanza vibaya, lakini mambo yakawa tofauti, kwani baada ya Rostov kupata bao la kuongoza kupitia shuti la mpira wa adhabu la Timofev Kalachev dakika ya 72, Eto’o alisawazisha baada ya kupata nafasi pekee usiku huu na kudhihirisha kwamba bilionea Suleyman Kerimov hakukosea kumwaga pesa chafu kwa ajili yake.
Dau rasmi la Eto'o kwenye klabu hiyo halijatajwa, lakini taarifa za vyombo vya habari zimesema inawagharimu Anzhi kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 39 huku mchezaji huyo akikunja mshahara wa dola Milioni 29 kwa mwaka.    

Comments