TAJI LA TATU LANUKIA MEXICO


Reyes wa Mexico akishangilia bao
BOGOTA, Colombia

Mexico ipo katika nafasi ya kutwaa taji lake la tatu kubwa mwaka huu, baada ya kuifunga Colombia mabao 3-1 jana hivyo kufuzu nusu fainali ya Kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20.
Timu ya wakubwa ya Mexico ilitwaa ubingwa wa Gold Cup Juni mwaka huu, ikiifunga Marekani 4-2 kabla ya kutwaa Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 Julai mwaka huu ikiifunga Uruguay 2-0 kwenye fainali.
Sasa Mexico itamenyana na ama Hispania au Brazil, ambazo zinakutana kwenye Robo Fainali leo.
Katika robo fainali nyingine jana, Ureno iliwatoa mabingwa mara sita Argentina kwa penalti 5-4kufuatia sare ya bila kufungana ndania ya dakika 120.

Comments