SPORTS WOMAN -MISS TANZANIA KUSAKWA KESHO

LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

26 Agosti 2011

VODACOM MISS TANZANIA 2011 SPORTS DAY
Shindano lingine dogo la kumtafuta Mrembo mwanamichezo [Fast Track – Top Sport Woman ] litafanyika Jumamosi katika ufukwe wa Jangwani Sea Breeze kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Mshindi wa shindano hilo atajipatia nafasi ya kuingia moja kwa moja katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya urembo ya Vodacom Miss Tanzania 2011.
Tayari warembo wawili wameshapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya mashindano haya. Warembo hao ni Mwajabu Juma aliyeshinda taji la Top Model na Tracy Sospeter aliyeshinda taji la Miss Photogenic.
Mbali na shindano hili dogo, mashindano mengine yaliyobaki ni Mrembo mwenye Vipaji, [Miss Talent] na Mrembo mwenye Mvuto, [Miss Personality] ambapo mshindi wake hutangazwa kila wiki kabla ya Fainali za Taifa zilizopangwa kufanayika tarehe 10 Septemba 2011 katika ukumbi wa Mlimani City.
Katika siku ya Michezo hapo Jumamosi warembo watashindana katika michezo mbalimbali ikiwemo:-
1) Riadha – Mita 100
2) Mbio za magunia – mita 100
3) Kuogelea
4) Kuruka chini – Long jump
Michezo mingine ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, n.k.
Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 linadhaminiwa na VODACOM,REDDS ORIGINAL,NEW HABARI [2006] LTD,STAR TV,GIRAFFE HOTEL na PAPA ZEE ENTERTAINMENT.

HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.

Comments