SNEIDJER AWAKATA MAINI ARSENAL, MAN UTD

KIPIGO ilichopata Arsenal kutoka kwa Manchester United, inaonekana kiliwachanganya zaidi mabosi wa timu hiyo, ambao waliamua kufanya kazi usiku na mchana ili kumtwaa kiungo wa Inter Milan, Wesley Sneijder. Sneijder ambaye alikuwa tangu awali akidaiwa kwenda Manchester United au City, alijikuta akiingizwa katika dili la kuuzwa Arsenal, ili kuwahi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Pamoja na mchezaji huyo kulipwa kiasi cha pauni 250,000 kwa wiki ndani ya San Siro, lakini Wenger alimtaka atue hapo kwani aliamini ujio wa jina kubwa itasaidia kurejesha imani kwa mashabiki.
Lakini Sneijder aliamua kuikata maini Arsenal na kusema hataki na wala hana mpango wowote wa kwenda katika timu hiyo na kutaka wamuache kabisa.
“Nitabaki Inter, siwezi kwenda, maana siamini unaweza kuhama katika aina hii, heri nibaki hapa,” alisema.

Comments

  1. muandishi .. ni arsenal hater.. jamaa hajawahi kutamka maneno hayo tumefuatilia usjili live sky news hadi dirisha linafungwa...

    jamaa kama kuwakata maini amewakata MAN UTD .. kama wenger ameshindwa kumlipa arteta pesa ambayo aliyokuwa analipwa everton sidhani kama alikuwa na interest na huyu ambaye analipwa mapesa mengi hivi

    ReplyDelete

Post a Comment