SIMBA YATOKA SARE NA LEOPARD


SAFU ya ushambuliaji ya Simba imezidi kumwangusha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mganda Moses Basena, baada ya jana kushindwa kufunga bao hata moja, dhidi ya FC Leopards ya Kenya, ambapo mpira ulikwisha kwa timu zote kutoka suluhu, mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha.

Katika mchezo wao wa kwanza wa kirafiki ambao ulichezwa kwenye tamasha la Simba Day, Wekundu hao wa Msimbazi walifungwa bao 1-0 na Victors ya Uganda, huku Basena akiwamwagia lawama washambuliaji wake kwa kukosa mabao mengi ya wazi.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofumania nyavu za mwenzake, hata hivyo Mike Barasa wa FC Leopards amekuwa akiisumbua ngome ya Simba. Katika kipindi hicho cha kwanza timu zote mbili zilikuwa zikishambuliana kwa zamu.

Comments