SIMBA YAPIGWA KIDUDE SIMBA DAY


SIMBA jana ilisherehekea vibaya tamasha lake la Simba Day baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Victors ya Uganda.

Mchezo huo wa kirafiki kusherehekea tamasha hilo ulifanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kuhudhuriwa na mashabiki mbalimbali wa soka.
Victors ilipata bao hilo pekee dakika ya 70 kwa mkwaju wa penalti mfungaji akiwa Patric Sembuya baada ya beki Victor Costa kumwangusha Suleiman Jtingo alipokuwa akielekea kufunga.
Washambuliaji wa Simba, Gervas Kago, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji haukuwa mzuri.
Nafasi ambayo Simba itaijutia zaidi ni ile ya dakika ya 15, wakati Moshi akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga alipiga shuti lililopaa juu ya lango.
Waganda walionesha uwezo mkubwa katika mchezo wa jana na kuutawala kwa kiasi kikubwa kiasi cha kuonekana kana kwamba wao ndiyo wenyeji.
Simba ilitumia tamasha la jana pamoja na mambo mengine kutambulisha wachezaji wake wapya itakaowatumia kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa.
Simba: Juma Kaseja, Salum Kanoni, Nassoro Masoud, Obadia Mungusa/ Kelvin Yondani, Victor Costa, Patrick Mafisango/Abdalah Seseme, Gervas Kago/Uhuru Selemani, Shomari Kapombe, Felix Sunzu/Rashid Ismail, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi.



Comments