SIMBA, YANGA DIMBANI LEO


VIGOGO vya soka nchini timu za Simba na Yanga leo vinashuka katika viwanja tofauti katika muendelezo wa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania Bara.
Mabingwa watetezi Yanga watashuka katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro kukwaana na Moro United, huku Simba itakuwa katika dimba la Mkwakwani, Tanga kukipiga na wenyeji Coastal Union ya huko.

Comments