SIMBA YAAGWA KWA SAFARI YA ARUSHA SIMBA DAY

WANACHAMA wa Simba wa tawi la kituo cha mabasi cha Ubungo wameisafirisha timu hiyo kwenda Arusha kwenye tamasha la 'Simba Day' litakalofanyika Jumatatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Wanachama hao wakiongozwa na Katibu wao Mkuu Justine Mwakitalima walichanga kiasi cha Ths 1.3 milioni na kukodi basi jipya la Kampuni ya Happy Nation aina ya Yutong kwa ajiri ya safari hiyo.
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam Makitalima alisema fedha hizo ni kwa ajiri ya safari ya kwenda tu na kwamba gharama za kurudi zitaandaliwa wakiwa jijini hapo.
Hizi ni gharama za safari tu ambazo tumekodi basi jipya kabisa na baada ya kufika Arusha tutaandaa usafiri mwingine kwa ajiri ya kurudi jijini Dar es Salaam,î alisema Mwakitalima.
Kuhusu gharama za chakula na malazi ya wachezaji hao wakiwa jijini Arusha alisema hilo wameliachia uongozi wagharamie na kwamba wangeweza kubeba jukumu lote la timu hiyo ila kwa sasa tawi hilo bado changa.
Mbali na gharama za usafiri pili tumewapatia maji ya Kilimanjaro katoni tano kwa ajili ya matumizi ya njiani, tufikia hapo kwa sasa kwa sababu tawi letu bado changa lina miezi sita tu tangu lilopo anzishwa lakini kwa siku za usoni tutaweza kugaramia kila kituîalifafanua Mwakitalima.
Wanachama wa tawi hilo wanajiandaa kwa safari ya kwenda Arusha kwenye sherehe hizo ikiwa na msafara wa watu 42.
IMETOKA GAZETI LA MWANANCHI

Comments