SIMBA WAIBA MCHEZAJI ZANZIBAR

KLABU ya Super Falcon ya Zanzibar iliyopanda daraja msimu wa 2011/2012 visiwani humo, imeishitaki klabu ya Simba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kitendo cha kumsajili mchezaji wao Edward Christopher Shijja katika kikosi chao cha vijana (Simba B) kinyume cha utaratibu.

Akizungumza kwa simu jana kutoka Zanzibar, Katibu wa timu hiyo, Khamis Bilal, alisema mchezaji wao alikuwepo katika kikosi cha Simba ambacho kiliweka kambi Zanzibar na kucheza mechi ya kirafiki na timu ya vijana ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 23, Julai 30 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Mao dze Tung ambapo aliingia kipindi cha pili.
“Nina ushahidi wa kutosha kwa sababu tulikuwepo uwanjani siku hiyo, Shijja alivaa jezi namba 28, tulivyoona hivyo hatukukaa kimya tuliiandikia barua Simba na kuwataarifu kuwa Shijja ni mchezaji wetu halali, lakini hawakutujibu kitu, ndipo tulipopeleka malalamiko yetu TFF ili watusaidie,”alisema.

Comments

  1. Maneno ya mkosaji kwa hao jamaa kwani Edward ana misimu karibu mitatu pale simba na kule kwao alikwenda kupiga daiwaka na alipomaliza nao makubaliano yao akatembea zake kurudi kazini kwake msimbazi sasa sijui wao walimsajiria wapi huyu dogo......

    ReplyDelete

Post a Comment