SIMBA SC WATUA MJENGONI, WAPONGEZWA


PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

MABINGWA wa ngao ya Jamii, timu ya Simba ya jijini Dar es salaam wametinga  bungeni na ngao yao hiyo waliyoipata baada ya kuwafunga mahasimu wao wa jadi, Yanga kwa mabao 2-0.

Baada ya kuwasili bungeni kwa timu hiyo,  shughuli za bunge zilisimama kwa takriban dakika moja kutokana na wabunge kuishangilia huku Spika wa Bunge Anne Makinda aliwakaribisha 'wekundu' hao na kuwapongeza kwa ushindi huo.
"Nawapongeza kwa ushindi wenu wa jana pamoja na ule mlioupata hivi karibuni kwa kuwafunga Yanga na kutwaa ngao ya hisani" alisema Makinda
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Ismail Aden Rage, alimkabidhi Nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja fedha zilizochangwa kwa lengo la kuipongeza timu hiyo kwa kutwaa ngao ya Jamii na wabunge wanaoishabikia timu hiyo, hata hivyo haikujulikana wachezaji hao walichangiwa kiasi gani cha fedha.
Baadhi ya wabunge na wanachama wa timu hiyo walipata fursa ya kupiga picha na wachezaji pamoja na viongozi wa timu hiyo huku wakiwataka waendelee kufanya vizuri kwenye mechi za ligi kuu zinazoendelea hivi sasa.

Comments