SIMBA NA AFC LEOPARD JUMAMOSI ARUSHA

SIMBA inatarajiwa kushuka dimba Jumamosi kucheza mechi ya kujipima nguvu na AFC Leopard ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema timu hiyo itakuwa Arusha na itarudi jijini saa chache kabla ya mechi yake ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumatano ijayo. Simba ilienda Arusha kwenye tamasha lake la Simba Day ambapo ilicheza na Victors ya Uganda na kuchapwa bao 1-0.

Comments