SIMBA NA AFC LEOPARD ARUSHA LEO


SIMBA leo watacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Kocha wa Simba, Moses Basena anataka kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga hapo Agosti 17, baada ya kufungwa na Victors ya Uganda kwa bao 1-0 kwenye tamasha la Simba Day.
Akizungumza kuhusu mchezo huo kocha Basena alisema anatumia mechi hiyo ili kuangalia mapungufu na jinsi wachezaji wake walivyobadilika kiuchezaji kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii.Basena alisema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri isipokuwa Mwinyi Kazimoto ambaye ni majeruhi na anatarajia mchezo wa leo utampa nafasi nzuri ya kutambua kikosi hicho licha ya kufungwa katika mchezo wa awali na Victors.



Comments