SIMBA KUGOMEA MECHI YA YANGA!

KLABU ya soka ya Simba imetishi kugomea mechi yake ya kuwania ngao ya jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga inayotarajiwa kupigwa jumatano kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Simba imefikia hatua hiyo ikishinikiza kamati ya KAtiba, Sheria na Haki za wachezaji  ya TFF imuidhinishe kiungo wake wa kimataifa, Gervas Kado ambaye aliidhinishwa na kamati ya mashindano kuichezea Simba kabla ya kuondolewa na kamati ya Katiba.
Kwa mantiki hiyo, Simba inadai haitakuwa tayari kushuka katika dimba hilo bila ya kurejeshwa kundini kwa mschezaji wake huyio aliyesajiliwa kutoka Afrika ya Kati.

Comments