Senegal yaokolewa kwa DRC

RAIS wa Senegal, Abdoulaye Wade ameamua kukiokoa kikosi cha soka cha timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kuamua kutoa tiketi ya ndege kwa wachezaji walio nje ili waweze kuja kuivaa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mchezo wa kufuzu wa Kombe la Mataifa Afrika. Wade, aliamua kuingilia kati na kuokoa mtafaruku uliokuwa umejitokeza kati ya Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) na wachezaji ambao wako nje ya nchi hiyo, ambao walikuwa hawajatumiwa tiketi za ndege.
Wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya nchi hiyo, waliamua kugoma na kutaka kwanza watumiwe tiketi kwani mara nyingi wanajikuta wanatumia fedha zao bila kurudishiwa.
Senegal inatarajiwa kukutana na DRC mwishoni mwa wiki katika mchezo unaotarajiwa kufanyika Dakar, ambao ndio pia utakaoamua timu itakayofuzu katika fainali hizo kutoka Kundi E.

Comments