KENYA WAMZUIA SANTO KUREJEA SIMBA

JERRY SANTO
KIUNGO wa Simba Jerry Santo ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, harambee Stars ambacho kitacheza na Botswana Agosti 10, mwaka huu mjini Gaborone.
Santo amerejea Nairobi kutoka Malaysia alipokwenda kusaka timu ya kuchezea na wakati akiwa na wito wa Harambee klabu yake, Simba imesema kwamba atajiunga na wenzake Jumapili.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga alikaririwa akisema jana jijini Dar es Salaam kwa kusema ni kweli kiungo huyo alienda kufanya majaribio nchini Malaysia ingawa alikiri hakutoa taarifa ya kufanya hivyo kwa klabu hiyo.
“Ni kweli Jerry alienda Malaysia kufanya majaribio ingawa hakuwa ametujulisha hilo kabla ya kufanya hivyo, lakini hilo linawezekana kwa sababu katika mkataba wake na Simba amebakiza miezi miwili tu,” alifafanua Kamwaga. Santo hakucheza mechi na Yanga fainali ya Kagame kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi na klabu yake ikafungwa 1-0.

Comments