VAN PERSIE NAHODHA MPYA ARSENAL


ROBIN Van Persie amemrithi Cesc Fabregas aliyehamia barcelona kama Nahodha ndani ya klabu ya Arsenal kuanzia leo Jumanne, lakini hatoiongoza timu hiyo katika mechi ya leo ya Champions League play off dhidi ya Udinese kutokana na kusimamishwa na UEFA.

Van Persie, 28, hatoweza kuitumikia klabu yake katika mechi ya leo katika uwanja wa Emirates kwa sababu amefungiwa kucheza mechi moja kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa mtoano dhidi ya Barcelona msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi itabidi asubiri mpaka Jumamosi katika mechi ya EPL dhdi ya Liverpool kwenye uwanja wa Emirates ili aweze kuvaa rasmi kitambaa cha unahodha.
Van Persie ambaye amekuwa Arsenal kwa takribani miaka 7 aliuambia mtandao rasmi wa Arsenal: “Kama nahodha unatakiwa kuwa balozi wa klabu na nipo tayari kwa jukumu hilo.
“Nimekuwa kwenye huu mchezo kwa zaidi ya miaka 10, hivyo natambua hii dunia inaendaje.Nilipokuwa na miaka 18 sikuwa na nafahamu kitu kuhusu uongozi lakini sasa nina uzoefu, hivyo naamini nipo tayari kwa jukumu.
Van Persie sio mtu pekee aliyefungiwa na UEFA, kocha Arsene Wenger nae yupo katika adhabu kutokukaa kwenye benchi kwa mechi moja baada ya kuadhibiwa na na UEFA kutokana maoni aliyoyatoa kuhusu refa Massimo Busacca kufuatiwa kutolewa kwa red card kwenye dhidi ya Barcelona mwezi wa 3 mwaka huu.


Comments