RAGE AMFUNGIA SAFARI KAGO, WACHEKELEA KUSHUKA DIMBANI KESHO

MWENYEKITI wa simba Alhaj Ismail Aden Rage yupo nchini Afrika ya Kati akifuatilia kwa ukaribu suala la mchezaji wake wa kimataifa Gervais Anold Kago.
Msemaji wa Simba Ezeckiel Kwamwaga amesema leo kwamba Rage amekwenda huko ili kuweza kuonana na viongozi wa klabu ya OLympic Real De Bangue aliyopkuwa anaichezea Kago baada ya kuwa kimya kuhusiana na suala la usajili wa mchezaji huyo.
Katika hatua nyingine, Simba imepokea kwa furaha taarifa za kurtuhusiwa kucheza mechi ya ngao ya jamii kesho katti yao na Yanga kwa kiungo mshambuliaji wake Kado, hivyo wamewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo.

Comments