POULSEN ATAJA SABABU ZA KUTOFANIKIWA KATIKA SOKA

KOCHA  mkuu wa Timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ Jan Poulsen amesema  kuwa nidhamu mbovu ndani na nje ya soka ni moja ya sababu zinazopelekea soka la Afrika hususani Tanzania kushindwa kupata mafanikio.
 Poulsen amesema, mbali na hilo suala jingine linalochangia kuwepo tofauti ya soka baina ya Afrika na Ulaya ni mbinu za kiuchezaji pamoja na mfumo wa uongozi kwa ujumla.
Aidha, Poulsen alisema nafasi ya Tanzania kupenya katika fainali hizo ni ndogo sana lakini indapo Stars itafanikiwa kushinda mechi zake mbili zilizisalia ikianza na hiyo ya Algeria na kisha dhidi ya Morocco, huku akiamini kikosi chake kinaweza kufanya mambo mazuri.

Comments