PILIKA ZA USAJILI LEO ENGLAND

Saa 11: 22: Wigan Athletic inamsajili winga Albert Crusat kutoka Almeria ya Hispania kwa mkataba wa miaka miwili.

Saa 11:11: Arsenal inatangaza wamekubali kumsajili mshambuliaji Chu Young Park kutoka AS Monaco ya Ufaransa.
Saa 11:05: Vladimir Weiss anaondoka Manchester City na kujiunga na Espanyol ya Hispania kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja. Saa 10:11: Beki Joleon Lescott anazungumzia uwezekano wa kiungo wa Manchester United, Owen Hargeaves kujiunga na Manchester City.
Saa 9: 35: Per Mertesacker alikuwa njiani kuelekea London jana kwa ajili ya vipimo tayari kuanza kazi Arsenal.
Saa 9:30: Wayne Rooney anazungumzia mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Owen Hargeaves kuwa mbioni kutua Manchester City.
Saa 9: 20: Owen Hargreaves anapigwa picha akiwa katika hospitali ya Bridgewater ambako wachezaji wa Man City wanapata huduma ya tiba, akiwa na daktari wa klabu hiyo.
Saa 9:17: QPR inaweza kutumia mwanya wa Stoke City kushindwa kumnasa Peter Crouch, kwa kukata dau la pauni Milioni 11 ili imnase.
Saa 915: Stoke inashindwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji mpya wa Chelsea, Romelu Lukaku.
Saa 8: 50: Mshambuliaji wa Liverpool, Joe Cole yuko mbioni kuhamia kwa mkopo wa msimu mmoja katika klabu ya Lille ya Ufaransa.
Saa 8:48: Kinda wa Fulham, Cheick Toure anajiunga na FC Lorient ya Ufaransa.
Saa 8:18: Beki wa kushoto wa Arsenal, Armand Traore anasaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na QPR.
Saa 8:10: Aston Villa inajenga matumaini ya kumnasa kwa dau la pauni Milioni 3, beki wa Spurs Alan Hutton baada ya kumuuza Luke Young kwenda QPR.
Saa 7:42: Newcastle United ipo kwenye mazungumzo na kipa wa Charlton, Rob Elliot.
Saa 6:45: Kiungo wa QPR, Shaun Derry amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2013.
Saa 5:57: Kiungo wa Inter Milan, Wesley Sneijder anatarajia kubaki Serie A msimu huu, kufuatia kuondoka kwa Samuel Eto'o aliyehamia Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Saa 5:41: Beki wa kushoto wa Inter Milan, Davide Santon anafanyiwa vipimo Newcastle.
Saa 5:17: Liverpool inakataa ofa ya pauni Milioni 8 pamoja na Yossi Benayoun ili kumtoa Raul Meireles Chelsea.
Saa 3:13: Arsenal inajiandaa kumsajili beki wa kushoto wa Brazil, Andre Santos kutoka Fenerbahce kwa dau la pauni Milioni 6.2.

Comments