PIGO SIMBA, ULIMBOKA NJE WIKI MBILI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Ulimboka Mwakingwe atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili kutokana na maumivu yanayomsumbua. Kiungo huyo aliyerejea Simba msimu huu baada ya kuachwa msimu uliopita na kwenda kuichezea Majimaji aliumia hivi karibuni kwenye mazoezi ya timu hiyo visiwani Zanzibar, ambako Simba imeweka kambi.
Hata hivyo habari njema kwa wana Simba ni kwamba, kiungo Mwinyi Kazimoto aliyesajiliwa msimu huu kutoka JKT Ruvu anaendelea vizuri. Simba itacheza na Yanga Agosti 17, katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii, maarufu Ngao ya Hisani.

Comments