PATA MISTARI YA WIMBO MPYA WA HUSSEIN MACHOZI 'UNANIFAA' REMIX

"UNANIFAA (REMIX)" LYRICS by HUSSEIN MACHOZI FT. C-SIR MADINI & SAGNA


Song title: UNANIFAA (REMIX)
Artists: HUSSEIN MACHOZI FT. C-SIR MADINI & SAGNA
Song written by: HUSSEIN MACHOZI, JOSEFLY & KID BWOY
arranged by: KID BWOY
Produced by: AMBA & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
AUGUST 2011

Verse 1 (C-sir Madini):
Bado mi najiuliza alobatiza hisia za moyo jina mapenzi weweee,
kwani mi lanitatiza mpaka najikuna pasipowasha kisa wewee,
nilipokuwa mi mdogo nilipohisi njaa, niliweza kutamka mama mi nanjaa,
ila leo mi mkubwa nahisi mapenzi, tatizo moja kusema neno nakupenda,
iliniuma sanaaa, uliponieleza hisia zako kwa yuleeee,
ukaniomba ushauri wa bure, wakati nami nakupenda zaidi ya yuleee eeh heee,
kweli inaniuma sanaaa, kuona tayari umeanza mapenzi na yuleee,
na nilivyo bwege wa karne, mimi mwenyewe niliekushauri umkubaliee eeh hee,
Bridge:(C-sir):
C-sir nimependa, ila nashindwa kukutamkiaaa,
nabaki tazama, nakula kwa hisiaaa,
C-sir nimependa, ila nashindwa kukutamkiaaa,
nabaki tazama, nakula kwa hisiaaa baby,


Chorus (Hussein Machozi):
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,
Verse-2 (Hussein Machozi):
Hisia zangu zinanitesa hadi nakondaaa,
mbaya zaidi napokuona moyo unadundaaa,
natamani ungejua nini nawazaaa,
labda ingekuwa rahisi mi kukupataaaa,
taswira ya sura yako inanijiaaa,
ndo maana siachi kuwaza kila napokwendaaa,

Bridge:(Hussein):
Nahisi napenda, ila nashindwa kukwambiaaa,
nabaki tazama, nakula kwa kuonaaa,
Nahisi napenda, ila nashindwa kukwambiaaa,
nabaki tazama, nakula kwa kuona eeei eeh,


Chorus (HUSSEIN MACHOZI):
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,
Verse-3 (Sajna):
Wingi wa nyuki kwa mzinga hauongezi utamu wa asali,
japo mi fundi wa maneno lakini kwako sina hali,
mara ya kwanza kwenye facebook, sajna sajna naomba urafiki,
sina hiyana mimi mtu wa watu, nawe ukawa wangu rafiki,
kimoyomoyo mi nasema nakupenda ah ah,
kwa sauti nashindwa kutamka,
moyo wangu hauwezi acha kukupenda ah ah,
mdomo unashindwa kutamka,
nimetumia lugha ya vitendo lakini nimepata zero,
nimejituma kuonesha upendo lakini huoni mi hero,


Bridge:(Sajna)
oooh oh kama sifaa, zote nakupa mama, wewe unanifaa wewe unanifaa sana mimi,
oooh oh kama sifaa, zote nakupa mama, wewe unanifaa wewe unanifaa sana mimi,


Chorus (Hussein Machozi & Sajna):
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,
Kama sifaaa, zote nakupaa,
ama kwa hakika, unanifaa,


END

Comments