OWEN ATUA MAN CITY

MANCHESTER CITY imeishitua dunia baada ya jana kukamilisha taratibu zote na kumtwaa aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Owen Hargreaves. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United, alifanyiwa vipimo vyote kuhusu afya yake na baada ya kufuzu akasainishwa mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Hargreaves alikuwa hana timu, baada ya Manchester United kuamua kumuacha mara baada ya msimu uliopita kumalizika na kwa miaka mitatu alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara.
Awali West Bromwhich Albion ilishampa ofa ya kwenda kuichezea, lakini aliamua kukaa kimya na kusubiri mpaka dakika za mwisho ili kuona kile kitakachotukia.
Kocha Roberto Mancini anaonekana kutaka kuimarisha zaidi kikosi chake kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu ambao unaonekana kuwa wa ushindani mkubwa.

Comments