NYOTA NBA ASAIDIA KWA LOWASSA


NYOTA wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA Dwight David Howard anayechezea timu ya Orlando Magic jana alitoa msaada wa dola za Kimarekani 60,000 zaidi ya Sh. Milioni 90 za Tanzania katika shule ya sekondari Kipok Girls iliyopo Monduli, Arusha.Howard aliyezaliwa Desemba 8, mwaka 1985 alikabidhi msaada huo mbele ya Mbunge wa jimbo la Monduli, Edward Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania.
Howard, ambaye hucheza nafasi ya katikati na ushambuliaji, yuko nchini kwa mwaliko wa taasisi moja iliyomwalika kwa ajili ya kusaidia shule hiyo na mwenyeji wake ni Lowassa.
Mchezaji huyo aliyechaguliwa mara tano kwenye All-Star za NBA, mara tano timu bora ya NBA na mlinzi bora wa mwaka mara tatu, mwaka 2008 alikuwemo kwenye kikosi cha Marekani kilichotwaa Medali ya dhahabu ya Olimpiki.
Kutoa misaada kwa jamii ni desturi yake, kwani Novemba mwaka 2009, aliingia kweney orodha ya watu katika kuwaia tuzo ya kufanya kazi za kijamii ya Jefferson (Jefferson Awards for Public Service), ambayo ni maalum kwa wanamichezo wanaofanya kazi za kijamii.

Comments