NI BRAZIL NA URENO FAINALI KOMBE LA DUNIA U-20

Henrique alifunga mabao yote mawili katika dakika 10 za mwisho na kuiwezesha Brazil kuitoa Mexico katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 20. Brazil sasa itamenyana na Ureno katika fainali.  Bao la mapema la kichwa la Danilo  na mkwaju wa penalti wa dakika ya 40 wa Nelson Oliveira uliipa timu ya Ilidio Vale(Ureno) ushindi wa  2-0 mjini Medellin, na kuitoa Ufaransa.

Fainali itapigwa Jumapili saa 10:00 usiku kwa saa za bongo wakati mchezo wa kusaka mshindi wa tatu utatangulia saa 7:01 usiku kwa saa za kwetu. wadau jitahidini muangalie new talents za dunia. Brazil v Ureno na Ufaransa v Mexico.

Comments