MUSTAFA HASSANALI AFANYA KWELI BOTSWANA

 Mbunifu,Mustafa Hassanali kutokaTanzania,akiongozana na mmoja wa wanamitindo,kuonyesha vazi la ubunifu,katika hafla ya Fashion Week,Gaborone,Botswana 13 August 2011
 mmoja kati ya wanamitindo,akionyesha vazi la ubunifu la Mustafa Hassanali kutoka Tanzania tarehe 13 august-2011,Gaborena Botswana
 mmoja kati ya wanamitindo,akionyesha vazi la ubunifu la Mustafa Hassanali kutoka Tanzania tarehe 13 august-2011,Gaborena Botswana

 mmoja kati ya wanamitindo,akionyesha vazi la ubunifu la Mustafa Hassanali kutoka Tanzania tarehe 13 august-2011,Gaborena Botswana
 
 
Mbunifu Mustafa Hassanali,ndio alikua mtanzania pekee aliealikwa kuwakilisha nchi yake katika wiki ya kwanza ya Fashion Botswana , iliyofahamika kama Color in the desert fashion week.

Hafla hii,iliudhuliwa na wabunifu mbalimbali wa kimataifa na wenyeji.Baadhi ya wabunifu wa kiafrika walioudhulia walikua , Taibo Bacar (Mozambique), David Tlale,na Thula Sindi kutoka Afrika kusini, Moo Cow (Kenya), Joyse Nyasha Chimanye( Zimbabwe). Kauli mbiu ya Fashion week mwaka huu,ilikua "Kuongeza tija na maendeleo ya fani ya ubunifu wa mavazi na viwanda vya nguo Botswana "
Mustafa Hassanali alisema "Kutokana na uzoefu wangu,Botswana ni nchi yangu ya kumi na moja kiafrika na ya kumi na tatu kidunia kufanya maonesho ya ubunifu,Na nnajisikia faraja na kujivunia kuwa mmoja wa walioudhulia week ya kwanza ya fashion Botswana,na pia kuwa mmoja wa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Botswana kupitia Fashion "


KUHUSU MUSTAFA HASSANALI

Mustafa Hassanali, mbunifu na mjasiriamali anaeamini katika “never say die” anatumia kipaji na ubunifu wake katika kuijenga leo na kesho katika ubunifu.

Kazi za Mustafa Hassanali zimethaminika kimataifa, ameweza kufanikiwa kuonyersha kazi zake zimeonekana katika majukwaa tofauti ya mitindo kama vile, Fashion Business Angola, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Africa Collection in Douala, Cameroon, India International Fashion Week 2009, Naomi Campbell’s Fashion for Relief 2009, Arise African Fashion Week 2009, Durban & Cape Town Fashion Weeks, Vukani Fashion Awards in Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival in Sicily, Italy, M’Net Face of Africa, Mozambique, Uganda na Kenya Fashion Weeks ambapo kwa pamoja yamemjengea kuheshimika sana.

Comments