MTAZAMO:TFF KUNA MATATIZO HIVI SASA SI BURE

MIAKA michache iliyopita, baada ya kilio cha muda mrefu juu ya uendeshaji wa mchezo wa soka hapa nchini, nafuu na nuru ilianza kuonekana.
Mafanikio hayo yalianza hasa pale Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilipoanza utekelezaji na utendaji wenye umakini katuika shughuli zake mbalimbali hata nuru kuanza kuonekana.
Lakini hivi sasa inasikitisha na ninajiuliza, kuna nini hivi sasa TFF?
Hivi karibuni tumeshuhudia zoezi la usajili likifanyika, lakini sasa yameanza kuibuka mambo ya ajabu ajabu, ambayo yanachafua na kutishia mustakabali wa soka letu.
Binafsi nikiwa mpenzi wa Yanga, nilipata nafasi hivi karibuni ya kumsikiliza Mwenyekiti wa klabu ya Simba, ambaye pia hivi sasa ana dhamana ya ubunge, Alhaj Ismail Aden Rage, alielezea kwa uzuri na uwazi kabisa baadhi ya taratibu za usajili hasa za mchezaji wao Gervas Kago, ziko wazi kabisa, kuwa unaweza kufanyika kwa ‘hard copy’ au ‘soft copy’.
Rage huyu huyu alipokuwa Tabora (TAREFA), alimsajili Haruna Moshi ‘Boban’ timu ya Mkoa, kulizuka utata na alipotaka kukata rufaa, tulielezwa wazi na muhusika wa TFF kutajwa kwa jina kabisa, kuwa ameagiza rufaa hiyo isipokelewe. Yaliyotokea wote tuliyaona na ikawa ikisemwa kuwa kuna hujuma za Yanga.
Sasa hivi usajili umemalizika, lakini TFF inaibua mambo yasiyo na tija, mfano Chuji ‘Athumani Idd’ Simba wamemalizana naye nay eye hana matatizo, lakini TFF inamlazimisha aingie kwenye malumbano.
Kwa mtazamo wangu, TFF kuna matatizo, kuna kitu hivi sasa, kumejaa ubabe, ubabaishaji na soka linazidi kuharibika.
Mfano hai hivi sasa, tangu aje Poulsen mafanikio hayaonekani kabisa, tofauti na ‘movie’ ile Maximo aliyokuwa ametuachia.
Kwa mtazamo wangu, vijana wazuri wachapa kazi tunao wapewe nafasi wafanye kazi, lakini sio hivi sasa mambo yanavyokwenda, TFF kuna matatizo.
TFF haielewi hizi klabu inazoziyumbisha na kuzisumbua bila sababu za msingi, zinatakiwa zishiriki ligi vema , kwani ndizo zinazokuja kuiwakilisha nchi kimataifa.
Kwa mtazamo wangu, TFF kuna tatizo hivi sasa na inapaswa lichukuliwe hatua za dharura kama kweli tunataka mafanikio katika soka letu.Mwandishi wa mtazamo huu amejitambulisha kwa jina la, Mzee Charles Komanya mkazi wa Musoma mkoani Mara na shabiki wa klabu ya Yanga. Anapatikana kwa simu namba: 0755 855 662.

Comments