MASHAUZI CLASSIC KUZINDULIWA EID EL FITR TRAVETINE HOTEL

MKURUGENZI MTENDAJI WA MASHAUZI CLASSIC, ISHA rAMADHAN 'MAMAA MASHAUZI' AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA UZINDUZI WA KUNDI LAKE JIPYA LA MUZIKI WA TAARAB AMBALO LITAZINDULIWA SIKU YA IDD MOSI.

HAPA AKITOA UTAMBULISHO WA BAAHI YA WASANII WANAOUNDA KUNDI HILO AMBAPO NDANI YAKE KUNA THABIT ABDUL, ISSA KAMONGO, RUKIA JUMA AMBAYE NI MAMA YAKE MZAZI NA WENGINEO

 WANAMASHAUZI CLASSIC
BAADHI YA WANAHABARI WALIOHUDHURIA HAFLA YA UTAMBULISHO WA KUNDI HILO


HUYU ANAITWA MZEE JUMA MBIZO AMBAYE NI MSHAURI MKUU WA KUNDI HILO

KUNDI jipya la muziki wa taarab nchini Mashauzi Classic ‘Wakali wa kujiachia’ linatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Eid El Fitr katika ukumbi wa Hoteli ya Travetine.

Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Isha Ramadhan ‘Mamaa Mashauzi’ aliwaomba mashabiki kuwaunga mkono.
Alisema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na ushindani uliopo katika tasnia ya muziki huo na hiyo inatokana na kuwa na wasanii waliosheheni vipaji vya hali ya juu.
“Tunaomba mashabiki wa muziki huu watupokee, tunawaahidi kuwapa burudani ya nguvu kuhakikisha mnakonga nyoyo zenu,”Alisema.
Isha aliongeza kuwa siku ya Idd pili watakuwa Kigamboni, Idd tatu watakuwa Kibaha, Idd nne watakuwa Kibaha na Idd tano watapiga ukumbi wa Wenge uliopo Ukonga.
Aliongeza kuwa mpaka sasa wameshakamilisha albamu mbili huku ile ya kwanza ikiwa na vibao kama Nani kama Mama, Baraka za Baba, Mamaa Mashauzi Mtoto kutoka Musoma na Umdhaniayendiye kumbe siye.
Kundi hilo linaundwa na wasanii 22 wakiwemo Isha mwenyewe, Rukia Juma, Thabit Abdul, Asia Juma, Rahma Maulid, Issa Kamongo, Zainab Machupa, Fatma Maulid, Hashim Said, Leyla Abdul na wengineo.

Comments