MASHABIKI WA AZAM FC KUKUTANA KESHO

Uongozi wa Azam Fans Club unawaarifu mashabiki wote wa Azam FC kuwepo kwa mkutano kwa mashabiki katika ukumbi wa Nouvel bar iliyopo Sinza Mori ubavuni mwa sheli ya Big bon.

Mkutano huo utakao fanyika agosti 14 saa 8 mchana katika ukumbi huo uliopo katika jengo la Nouvel bar Sinza Mori.
Mkutano huo utaanza saa 8 na robo ukiwa na agenda saba ambazo ni:
1. Kuandaa tukio la kuitambulisha Azam Fans Club.
2. Mchakato wa undwaji wa katiba ya Azam Fans Club.
3. Kuutengeneza muundo wa uongozi wa Azam Fans club.
4. Kiasi na namna ya utoaji wa ada ya uwanachama.
5. Idhini ya kutengeneza bank account.
6. Mchakato wa kutengeneza vikundi vya ushangiliaji.
7. Namna ya kuwatunuku wachezaji wa Azam FC waliofanya vyema katika kipindi husika.
Kumbuka mtaji wa timu wa soka ni mashabiki. Kujitokeza kwako ndio kufanikisha zoezi zima.

Comments