MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KATIKA FAINALI ZA MASHINDANO YA QUR-AN DAR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa fainali za mashindano ya Qur-an kuhifadhi Juzuu 30, zilizofanyika jana Agosti 14 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Mshindi wa kwanza katika fainali hizo alikuwa ni Mariam Salum Mohamed, kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa fainali za mashindano ya Qur-an,  kuhifadhi Juzuu 30, Aisha Faki Khatib (18), kutoka,  Istiqama  Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 96 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa  fainali za mashindano ya Qur-an,  kuhifadhi Juzuu 10 (Tahqeeq), Mohamed Salum (12) kutoka,  Darul ,  aliyeibuka na jumla ya Pointi 98 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Baraza Kuu la Kiislam (BAKWATA), Shamim Khan, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam jana Agost 14. Kulia ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.

Comments