MAJERUHI KIBAO YANGA SC

MABINGWA watetezi wa ligi kuu bara, timu ya soka ya Yanga wataianza vibaya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2011/2012 kutokana na wachezaji wake sita kuandamwa na majeruhi.
Ligi hiyo ambayo inaanza jioni ya leo katika viwanja tofauti huku Yanga ikitarajiwa kuanza kampeni yake kesho kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa kukwaana na JKT Ruvu.
Majeruhi hao  ni pamoja na Yaw Berko, Davies Mwape, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Kenneth Asamoah, Kiggi Makasi na Idrisa Rashid.
Hata hivyo, Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema, kukosekana kwa wachezaji hao siyo pengo kubwa kwenye kikosi hicho kutokana na kuwepo wengine wenye uwezo watakaoziba nafasi zao.

“Ni jambo la kusikitika kwenye kikosi chetu, kutokana na idadi ya majeruhi kwenye kikosi chetu kuongezeka, na kufikia sita hadi sasa hivi ambao wataikosa mechi ya leo dhidi ya JKT Ruvu.
“Wachezaji watatu ambao ni Asamoah, Cannavaro na Asamoah walipata majeraha kwenye mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Simba, Idrisa yeye aliumia mazoezin, Berko na Mwape hao wanaendeleza kuuguza majeraha yao ya muda mrefu.



Comments