PRESHA INAPANDA, PRESHA INASHUKA


MAHASIMU wa jadi nchini timu za simba na yanga watamaliza tambo za nani zaidi usiku wa leo watakapokutana kwenye mechi ya kuwania ngao ya jamii kwenye uwanja wa taifa,dar es salaam.Timu hizo zinakutana katika mechi hiyo ambayo pia ni mahususi katika kuzindua msimu mpya wa ligi kuu soka tanzania bara utakaoanza agosti 20.Yanga ambao wanashikilia ubingwa wa ngao hiyo wameapa kuendeleza ubabe kwa simba kama kawaida,ikumbukwe kuwa mara ya mwisho timu hizi zilikutana kwenye mechi ya fainali ya kombe la kagame ambapo yanga ilitwaa ubingwa kwa kushinda bao 1-0.Simba nao wamejinasibu ya kurejesha heshima yao kupitia mechi hii na kutwaa ngao hiyo.

Comments