MA- PRO SIMBA SC WATIMKA


OKWI

SANTO
WACHEZAJI wa kimataifa wa klabu ya soka ya Simba, Emmanuel Okwi, Patrick Mafisango na Jerry Santo wametimkia kwao baada ya kuitwa na timu za taifa zinazojiandaa kwa mechi za kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.
Wakati Okwi akiitwa katika timu ya taifa ya Uganda, Santo ameitwa timu ya yaifa ya Kenya  na Mafisango timu ya Rwanda.
 Simba itaanza mazoezi yake jumatatu kujiandaa na mechi yake yake ya Ligi Ku Bara dhidi ya  Villa Squad bila nyota wake hao, pamoja na wale wa ndani ambao wameitwa pia katika timu ya taifa, Taifa Stars.
Nyota wa Simba walioitwa Stars ambayo inaingia kambini leo kujiandaa na mechi yake na Algeria itakayopigwa Septemba 3 ni pamoja na Juma Kaseja, Amir maftah, Juma Nyoso, Victor Costa na Salum Machaku.

Comments