LYON YATAKA KUCHEZA SHINYANGA NA SIMBA, YANGA

TIMU ya soka ya African Lyon imewasilisha barua katika Shirikisho la soka la Tanzania TFF ya kuomba mechi zao za Simba na Yanga kufanyika mkoani Shinyanga. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa wamepokea maombi ya timu hiyo ili kutumia mkoa huo.
Wambura alisema kuwa maombi hayo yanaambatana na maombi ya Azam waliyowasilisha jana ya kuomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwa ajili ya michezo hiyo.
“Timu zote hizo zinataka kama wao ni mwenyeji basi mchezo wao uchezwe Mwanza kwa Azam huku African Lyon ikitaka Shinyanga,”alisema. Wambura alisema maombi ya timu zote hizo yanafanyiwa ambapo alihaidi kuyajibu maombi hayo mapema iwezekanayo. Hatua za timu hizo kuomba mchezo huo kuhamishiwa mikoani inakuija baada ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kufungwa kwa ajili ya kupisha marekebisho ya Uwanja huo.

Comments