KINA JJ WA SIMBA SC WATUA A -TOWN

MABEKI mahiri wa timu ya soka ya Simba Juma Jabu na Juma Nyoso wametua mjini Arusha kujiunga na wenzao waliopo kambini kujiandaa na mechi yao ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga itakayopigwa jumatano ijayo.
Wachezaji hao waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, wameungana na wenzao ambao wapo huko tangu mwishoni mwa wiki iliyopita wakiendelea na maandalizi pia ya msimu mopya wa ligi kuu soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20.
Katika sehemu yake ya maandalizi, Simba itacheza na AFC Leopards ya Kenya siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo.

Comments