KIIZA ATUA, YANGA SASA KAMILI

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Hamis Kiiza amerejea nchini jana na kuelezea sababu zilizomfanya kuchelewa kujiunga kwa muda muafaka na mabingwa hao, huku uongozi wa Simba ukipanga kumwadhibu kiungo Jerry Santos kwa kuchelewa.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uganda aliondoka nchini baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Kagame, lakini alishindwa kujiunga na kikosi cha Yanga kilichoanza mazoezi rasmi Julai 20 ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.Kiiza aliyetua Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 10.45 jioni kwa ndege ya Shirikala Ndege la Uganda alisema kilichosababisha kuchelewa kurudi kwake ni matatizo ya kifamilia yaliyomkabili.
"Ukweli ni kwamba mchumba wangu ni mjamzito na taarifa za madaktari zinasema anaweza kujifungua kwa operesheni(upasuaji), huu ni ujauzito wake wa kwanza, na mimi pia nilikuwa sijui jambo lolote kwa sababu sijawahi lolote.
"Pia wazazi wa mchumba wangu walikuwa hawanitambui, nikalazimika kwenda kwao kujitambulisha na kukamisha mambo yote ili baadaye niweze kufunga ndoa,"alisema Kiiza.

Comments