KALOU APIGWA BEI CHELSEA


KOCHA wa Chelsea, Andre Villas-Boas anataka kumgeuza mchezaji Salomon Kalou kama ‘mbuzi wa shughuli’ kwa kumpeleka Tottenham Hotspurs ili ampate Luka Modric.

Villas-Boas anataka kumtumia Kalou kama ngao ya kufanikisha azma yake ya kumtwaa Modric, ambaye kwa sasa Spurs imegoma kumuachia hata pamoja na kuwekewa dau kubwa mezani.
Mabosi ndani ya Stamford Bridge, tayari wameanza mazungumzo na wale wa Spurs juu ya kubadilishana wachezaji hao na kupewa kiasi kingine cha fedha.
Kocha wa Spurs, Harry Redknapp amesema wazi kwa sasa hawezi kumuuza mchezaji huyo, kwani anamuhitaji mno kuliko kitu chochote kile.
Modric pia kwa sasa amewashutumu viongozi wake wa Spurs kwa kutotaka kusikiliza matakwa yake ya kuhama ndani ya timu hiyo.

Comments