JLO NA DIDDY PENZINI TENA

Jennifer Lopez na P.Diddy wamekuwa wakitanua pamoja usiku Jijini New York City – hivyo kuibua tetesi za wawili hao kurudiana.

Wapenzi hao waliwahi kula raha kwenye bahari ya mahaba kwa miaka miwili na nusyu kabla ya Jennifer kuvunja uhusiano huo mwaka 2000, lakini vyanzo vinasema kwamba nyota huyo wa Latin Amerika amekuwa akitafuta namna ya kurudiana na rapa huyo mwenye umri wa miaka 41, baada ya kuachana na Marc Anthony Julai 14.

Comments