HUSSEIN MACHOZI AREJEA TETEMESHA RECORDS



TAARIFA RASMI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI KUREJEA TETEMESHA


Hello mdau,
Hii ni taarifa rasmi kwa media na wadau wote kuhusiana na HUSSEIN MACHOZI kurejea katika familia ya TETEMESHA RECORDZ, iliyomtengeneza na kumkuza kimuziki mpaka hapo alipo toka mwaka 2007.
Kumekuwa na taarifa nyingi hapo katikati lakini hii ndio taarifa rasmi na ya kweli kuwa yalitokea matatizo kidogo mwaka jana (2010) mwanzoni, yaliyotokana na Hussein kukiuka baadhi ya masharti ya mkataba wake na Tetemesha, yaliyopelekea uongozi kuamua kusitisha kwa muda mkataba wake ili kumpa nafasi ya kupewa nguvu msanii mwingine aliyekuwa ndio anaaza kutambuulishwa mwaka jana anayefahamika kama SAJNA. Baada ya kumtambulisha vizuri Sagna, mwaka huu pia Tetemesha tumeweza kumtambulisha msanii mwingine wa tatu aitwaye C-SIR MADINI.
Sasa tumeona ni wakati muafaka wa kumrudisha Hussein Machozi rasmi ndani ya Tetemesha baada ya kukaa nae chini na kufanya makubaliano mapya na kusaini mkataba mwingine toka katikati ya mwaka huu, isipokuwa tumechelewa kuwapa taarifa kwasababu tulikuwa tunaweka kwanza mambo kadhaa sawa.
NEW SONG:
Hussein Machozi akiwa chini ya Tetemesha Entertainment ameshaanza kurekodi baadhi ya nyimbo mpya zitakazotoka mwaka ujao 2012, lakini kwa sasa tunautambulisha wimbo wake ambao ni REMIX ya wimbo alioutoa mwaka jana unaitwa “UNANIFAA”.
Katika version ya mwanzo ya wimbo huo aliimba peke yake, lakini katika remix hii amewashirikisha wasanii wenzake wa Tetemesha ambao ni C-sir Madini na Sagna.
Unanifaa remix imeandikwa na Hussein mwenyewe verse yake na chorus, na verse za Sagna na C-sir zimeandikwa na mwandishi rasmi wa Tetemesha anaitwa JOSEFLY kwa kushirikiana na Kid Bwoy.
Version ya mwanzo ya wimbo huo ilifanyika Akhenato Records chini ya Lil Ghetto. Remix beat imefanywa na Amba, na vilivyosalia vyote vimefanyika Tetemesha Recordz.


CREDITS:
Artists: HUSSEIN MACHOZI FT. C-SIR MADINI & SAGNA
Song title: UNANIFAA (REMIX)
Written by: Verse-1: JOSEFLY, Verse-2 & Chorus: HUSSEIN MACHOZI, Verse-3: JOSEFLY & KID BWOY
Produced by: AMBA for TETEMESHA RECORDZ 2011
Vocals Recorded by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ (Mwanza).

Comments