HAKUNA WA KUNITETEMESHA

MMOJA Ya washiriki wa Shindano la kumsaka Miss Tanzania Loveness Flavian (Pichani) amejitapa kuwa hakuna mrembo yoyote anayemhofia kati ya waliopo kwenye kambi ya kujiandaa na shindano hilo lililopangwa kufanyika SEptemba 10 kwenye ukumbi wa mlimani City.


Mrembo huyo ambaye pia anashikilia taji la Miss Lindi na lile la Kanda ya Kati alisema na haki ya kujitapa hivyo utokana na kuwa warembo wote waliotinga hatua hiyo ni bomba hivyo ushindi unategemea na bahati utakayokuwa nayo.
"Kusema kweli mimi hata simuhofii mshiriki yoyote kwani wote tupo sawa na ndio maana tumefikia hapa, muhimu ni kufanya kazi ya ziada itakayoendana na bahati ili uweze kuibuka na ushindi,"Alisema.
Warembo 30 watawania taji hilo ambalo linashikiliwa na Geneviev Mpangala.

Comments