GERVINHO AFUNGIWA MECHI TATU

Mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho amefungiwa mechi tatu kufuatia kupewa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alitolewa nje baada ya kugombana na 'mtukutu' Joey Barton. The Gunners wamekata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Lakini Chama cha soka imetupilia mbali rufaa hiyo, maana yake nyota huyo wa Ivory Coast atatumikia adhabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyejiunga na Arsenal mwishoni mwa msimu akitokea Lilleya Ufaransa kwa dau la pauni Milioni 10.5, atakosa pia mechi dhidi ya Liverpool, Manchester United na Swansea.

Comments