FILBERT BAYI AULA IAAF

KATIBU mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi (pichani kushoto)amechanguliwa tena kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF).

Katika uchanguzi huo uliofanyika huko Korea Kusini, Bayi ambaye ni bingwa wa rekodi ya dunia wa zamani katika mita 1500, ndiye Mtanzania wa kwanza kupata nafasi hiyo.
Uchaguzi huo umekwenda sambamba na mashindano ya riadha ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanariadha mmoja, Zakia Mrisho anayekimbia mita 5000.

Comments