FABREGAS KWAHERI ARSENAL


NAHODHA wa Arsenal, Cesc Fabregas yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Mabingwa wa Ulaya, Barcelona kwa gharama ya uhamisho wa Pauni 35 milioni. Uhamisho huo uliotawala kwenye historia ya Ligi Kuu, lakini bado haujakamilika na Arsenal wanategemea kuukamilisha mwishoni mwa wiki hii.Kiongozi wa juu wa klabu hiyo, alisema fedha zote zitakazopatikana zitatumika kwa ajili ya kununulia wachezaji wapya.
Gunners imekuwa ikihusishwa na kutaka kuwasajili Scott Dann, Phil Jagielka na Gary Cahill.Kocha wa Gunners, Arsene Wenger yuko kwenye harakati kubwa za kutaka kuimalisha ngome. Hivyo anamtaka beki wa kati Dann (Birmingham), (Everton) Jagielka na Cahill wa Bolton.
Fabregas, 24, hatoweza kuichezea Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa kama ataichezea Arsenal dhidi ya Udinese hapo Jumanne, kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi.
BBC inaamini kuwa gharama ya Pauni 30 mil, pamoja na Pauni 5 mil zitakazolipwa baada ya kucheza, hakuna shaka kwamba Fabregas.Inaamini kama akiuzwa, klabu hiyo ya Hispania italazimika kulipa Pauni 4 mil kufidia Pauni 1 mil kwa mwaka kwa sababu ya kuvunja mkataba wa nyota huyo, lakini wanajiandaa kufanya mazungumzo juu ya hilo.
Kama Fabregas akikamilisha uhamisho huo, atakuwa mchezaji wa pili mkubwa wa Barcelona baada ya nyota wa Chile, Alexis Sanchez kuuzwa kwa Pauni 23 mil.





Comments