ETO'O GHALI ZAIDI DUNIANI

MCHEZAJI Samuel Eto’o kwa sasa amekuwa ni mchezaji ghali zaidi duniani, baada ya kufanikiwa kukamilisha mkataba wa kuichezea Anzhi Makhachkala akitokea Inter Milan. Katika mkataba huo wa uhamisho, Anzhi imelazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 22 (Sh bilioni 58), lakini itampa mshahara wa pauni milioni 18 (Sh bilioni 48) kwa mwaka, huku akipewa kiasi cha pauni 350,000
Wakala wa mchezaji huyo, Claudio Vigorelli alisema mkataba kati ya mchezaji huyo na Anzhi ulitarajiwa kukamilishwa jana usiku na tayari maafikiano ya kimsingi yamefikiwa.
Habari kutoka Urusi zinasema kuwa, mmiliki wa Anzhi, Suleiman Kerimov, si bilionea pekee aliyetia mkono wa kumtwaa huyo, bali pia kuna senata mwingine aliyechangia pia na kwa sasa wanamtaka beki wa Barcelona, Dani Alves.
Wakati huohuo, beki wa kimataifa wa Cameroon ambaye kwa sasa anaichezea Anzhi, Benoit Angbva, amekiri ndiye aliyemshawishi kwa kiasi kikubwa mchezaji huyo kutua hapo.
“Nilizungumza na Eto’o mwezi Juni na nikamueleza kila kitu kinachoendelea hapa, hivyo ujio wake una mchango mkubwa kutoka kwangu,” alisema.


Comments