EAST AFRICAN MELODY KUTOA BURUDANI MBAGALA SIKU YA IDD MOSI

BENDI ya Taarabu East African Melody Idd Mosi kitafanya onesho maalum katika Ukumbi wa Nawina Resorts uliopo Mbagala Kuu, Dar es Salaam.

Mratibu wa Onesho hilo Zahor Said, alisema kuwa maandalizi ya Onesho hilo yamekamilika.
Alisema katika onesho hilo Melody itakuwa na wanamuziki wake wote mahili ambao wamekuwa wakitamba na nyimbo mbalimbali.
Said alisema kabla ya onesho hilo ambalo litafanyika kuanzia saa 2:00 usiku, kutakuwa na muziki kwa ajili ya watoto ambao watapata zawadi mbalimbali.
Alisema burudani kwa watoto itaaanza saa 9:00 alasiri ambayo itamalizika saa 12:30 jioni.
"Tumeandaa zawadi kwa mbalimbali kwa watoto watakaocheza vizuri zawadi hizo ni vifaa mbalimbali vya shule...ni changamoto kwao kujitokeza"alisema Said.

Comments