COSTA RICA YANG'ARA WORLD CUP U-20

JOE CAMPBELL
Beki  John Ruiz alifunga bao la ushindi dakika ya 72 na kuifanya Costa Rica ishinde 3-2 dhidi ya Australia jana, na kuiwezesha kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 20.

Ushindi huo wa kwanza kwa Costa Rica kwenye michunao hii imewafanya watinge hatua ya pili kutoka Kundi C, kwa pointi zao tatu nyuma ya Hispania. Australia na Ecuador kila moja bado ina pointi moja baada ya kucheza mechi mbilimbili.

Mshambuliaji  Joel Campbell aliifungia bao la kuongoza Costa Rica katika dakika ya 22 kwenye Uwanja wa Palogrande kabla ya Tommy Oar kuisawazishia Australia dakika ya 26, lakini Campbell tena akafunga la pili dakika moja baadaye. Australia ilipata bao la kusawazisha baada ya beki Franciso Calvo kujifunga dakika ya 64, lakini bao la kichwa la Ruiz kutokana na krosi ya Campbell liliipa ushindi Costa Rica.

Comments