CHUJI SASA KUISIKIA KWENYE BOMBA LIGI KUU


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kama Simba imemkana Athumani Iddi ‘Chuji’, basi mchezaji huyo hatoweza kucheza Ligi labda asubiri usajili wa dirisha dogo Januari.  Kauli hiyo ya TFF imekuja siku moja baada ya Simba kusema kwamba Chuji si mchezaji wao kwani walishavunja naye mkataba na kumalizana na kumuuza kwa mkopo Villa Squad, ambayo amekwishajiunga nayo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, kamati ya Katiba, Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF ilisema kwamba Chuji ni mchezaji halali wa Simba licha ya jina lake kutoonekana kwenye orodha ya wachezaji wa Simba walioombewa usajili.



Comments